Baada ya kufanya collabo yake na Diamond(My number one) ilisemekana
kulikuwa kuna beef kali kati yao baada ya Davido kupost kitu ambacho
kilionyesha wazi kuwa alikuwa anaidiss Tanzania baada ya Idris
kutangazwa mshindi kwenye mashindano ya Big Brother Afrika. Davido
amekana Tuhuma hizo na amesema kuwa ujumbe ule ulikuwa hauhusu jambo
hilo.
Akihojiwa na Mtangazaji wa Clouds Fm Millardayo Davido amesema kuwa
hajawahi kuwa na bifu na Diamond Platnumz na anamchukulia kama kaka yake
tangu siku ya kwanza walipojuana, kaongeza kuwa watu huwa wanafanya
kila mbinu kugombanisha watu wakiona watu wako kwenye mafanikio.
No comments:
Post a Comment