24 July 2015

Afande Sele Amchana Sugu, Adai Hajafanya lolote Bungeni Kutetea Muziki, Sugu Ajibu

 
Rapper Afande Sele amesema wasanii hawajanufaika na ubunge wa Joseph Mbilinyi aka Sugu licha ya kumsaidia kumpigia kampeni katika uchaguzi uliopita.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio, Afande alisema Sugu ameshindwa kuwatumikia wasanii na kujinufaisha yeye mwenyewe.

“Sisi tuliamini akienda kule ndio mdomo wetu, kasahau kabisa wasanii wenzake,” alisema. “Kipindi ambacho wasanii wa antivirus wanalalamika kwamba kawatosa porini, akasema yeye sio mbunge wa wasanii ni mbunge wa Mbeya. Huyu ni msaliti kwa wenzake, sasa mtu msaliti namna hii jinsi kumuondoa ni sisi kuamua kuingia bungeni wenyewe kupigania maslahi yetu,” aliongeza.

Baada ya kauli hiyo, Sugu amemjibu kwa kusema kuwa yeye hakuwa mbunge wa wasanii bali alikuwa mbunge kwaajili ya watu wake wa Mbeya mjini.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname