Wema Sepetu ni mmoja kati ya wasanii ambao wamejitokeza kuwania nafasi ya Ubunge.
Ili kulifanikisha hili Wema Sepetu ameomba mchango wa hali, mali hata mawazo ili aweze kufikanisha azma yake ya kuingia Bungeni.
Kupitia Instagram Wema Ameandika:
"Uongozi
ni utumishi. Naamini kama kijana nina uwezo wa kutumikia vijana
wenzangu, mama zangu na nchi yangu kwa ujumla. Hili jukumu langu na letu
sote.
Nimeamua kwa dhati kuwatumikia wananchi wa Singida na nchi yangu kwa ujumla endapo nitachaguliwa na chama changu.
Ili
nifanikiwe katika hili nahitaji mchango wenu wa mawazo, hali na mali.
Najua kila mmoja ana mchango wake katika kulifanikisha hili.
Naomba
nitumie nafasi hii kuwaombeni wote michango yenu bila kujali itikadi,
jinsia, umri au kigezo chochote. Mchango wako wowote utatusogeza karibu
kufikia lengo letu. Tafadhali
kwa anayependa kuchangia anaweza kutuma mchango kupitia namba
+255655106538 ambayo imesajiliwa kwa Jina la Ahmed Hashim Ngahemela...
Asanteni sana...."
No comments:
Post a Comment