08 June 2015

SIWEMA AMWANGUKIA NAY WA MITEGO! MWENYEWE AFUNGUKA KIHIVI...

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa katika pozi na Siwema Edson. Kilidai kwamba hivi karibuni, mmoja wa dada wa Siwema (jina linahifadhiwa) amekuwa akimpigia simu Nay akimuomba arudishe moyo wake kwa Siwema, kwani tangu aachane naye mambo yamekuwa yakienda kombo ikiwemo ule msala wa kesi inayoendelea mahakamani ya kujipatia mali isivyo kihalali.Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni ndugu wa Siwema kilieleza kuwa, pamoja na maneno ya shombo aliyommwagia Nay wakati wanaachana, mrembo huyo kwa sasa ameweka silaha chini akiomba wawe kama zamani.
Mwisho wa jeuri? Mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson anadaiwa kumwangukia mwanamuziki huyo ili warudiane walee mtoto wao.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname