Alikiba ameelezea kusikitishwa kwake na taarifa iliyosambaa kuwa
alitoa kauli dhidi ya Diamond kuwa anajisikia kichefuchefu kila
akimsikia msanii huyo.
Akizungumza na Bongo5 jana, Alikiba alisema hata watu wake wa karibu wanajua hawezi kufanya jambo kama hilo.
“Hiyo mimi nimeisoma juzi na mwenyewe sijaifurahia. Vilevile na
kibaya zaidi inaonesha eti kwamba mimi nimesema nikimsikia Diamond
najisikia kichefuchefu, mimi namchukia Diamond,” amesema.
“Yaani kwa uelewa wangu na akili yangu timamu hata watu wanaonielewa
mimi hata uwezo wa kusema hivyo sina na siwezi, kibinadamu haipendezi.
Halafu huyu mwandishi aliyeandika hivi anamaanisha kabisa anapenda huu
uchochezi ulipo na mabifubifu na mateam team yanayoendelea ilimradi
nionekane mimi na sura mbaya katika jamii. Kwa sababu hicho kitu ni cha
kutukosanisha. Huwezi kuniandika mimi nimesema live halafu kulikuwa na
waandishi wengine wakati nahojiwa mbona hao waandishi wengine
hawakuandika hivyo?” amehoji Kiba.
“Ushahidi wa sauti upo bana, sio kwamba unakwenda unaandika habari
tofauti ilimradi nionekane mimi ni mbaya mbele ya watu. Mimi hicho
kitendo kimeniudhi na sijakipenda, sijakifurahia na hii inakuwa
inashusha hadhi ya kampuni kwa sababu siku nyingine watu wanavyotaka
habari tutaonyesha ushirikiano mdogo kwa sababu ya vitu kama hivyo.
Watu wanaalikwa vizuri kufanya kazi ili kuwafikishia wananchi habari
lakini habari zinazokwenda ni tofauti. Hii haipendezi na sijafurahishwa
nayo na nimesikia watu wanatukana sana wanaongea comment tofauti
tofauti.”
Katika hatua nyingine Alikiba alizungumzia kwa mara nyingine tena
kuhusiana na uadui katika mashabiki wake na wale wa Diamond kwenye
mitandao ya kijamii.
“Ukitaka kuzungumzia upande wa timu na unapande wa support, sisi
hatusaidiani kwa kweli in general, hatusaidiani kabisaa. Na ukizungumzia
upande wa team, mimi simaanishi na support hizi timu ziwepo na sina
nguvu yoyote ya kumzuia mtu kufanya anachojisikia, wameshindwa watu
wengi. Kulikuwa kuna ubishano wa mashabiki wa Simba na Yanga, ikija timu
pinzani wanashabikia timu pinzani hivi hivi tulikuwa tunajionea hapa.
Sina nguvu hiyo kwamba nitamkataza mtu kwa sababu simjui hata mmoja na
nani na nani ambaye anashabikia. Mimi chakuchangia ninaweza sema
tu-support vya kwetu hicho ndo kitu naweza kusema.”
No comments:
Post a Comment