25 June 2015

NAPE AZOMEWA, KINANA AMSHUSHA JUKWAANI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ameanza vibaya ziara yake wilayani Sengrema, Mwanza baada ya wananchi kumzomea. 
Tukio hilo limetokea jana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Zeno uliyopo Sengerema mjini, Mwanza. 
Katika mkutano huo, Nape alizungumza maneno yaliyowatibuwa wananchi hasa wale wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa UKAWA.
Kwenye kauli zake Nape ambaye yupo katika ziara moja na Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa, baadhi ya vijana wamekuwa wakipewa viroba ili wafanye fujo.
Nape aliwalaumu vijana hao kwamba, wanapewa pombe aina ya viroba na viongozi wa vyama vya upinzania ili kwenda kufanya fujo katika mikutano ya chama hicho tawala.
“Chadema kimechoka sasa hivi lakini nyie vijana bado mmeng’ang’ani tu, mnapewa viroba na vikisha panda mnashikilia bendera ya ‘Peoples Power’ bila kufahamu kwamba, chama chenu kimeisha poteza mwelekeo.
“Kuna watu wanasema eti CCM ifungashe vilago vyake katika Wilaya ya Sengerema kwa kuwa Chadema inaingia katika uchaguzi huu, hicho kitu hakitawezekana na wao ndio wataondoka, mtang’ang’ania sana,” amesema Nnauye.
Kauli hiyo iliyosababisha baadhi ya wafuasi wa Chadema kuanza kuzomea na hata kusababisha mkutano huo kusimama kwa saa moja.
Hata hivyo, Kinana hakuweza kuvumilia hali hiyo na kuamka kutoka sehemu aliyokuwa amekaa na kumfuata Nape kumwambia ashuke kutoka jukwaani na kutumia nafasi hiyo kuwaomba radhi wananchi hao.
Katika hatua hiyo, Kinana alitumia nafasi hiyo kuwaweka sawa wananchi hao kuwa CCM ipo imara na haitetereke kwa chochote na kwamba, itatumia kanuni na misingi ya chama hicho katika kuijenga nchi na kuleta maendeleo.
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimekuwa na nguvu kubwa

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname