Nguo aliyoivaa usiku wa June 13 kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro kwa
nia ya kutoka kitofauti, imegeuka kuwa zimwi linalomtesa kiasi cha
kumfanya apokonywe mtoto wake kwa amri ya mahakama na mzazi mwenzake,
mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu. Faiza Ally
anajuta!
“Siwezi kurudia kosa, nitakuwa makini zaidi katika mavazi yangu,” Faiza
aliliambia gazeti la Mwananchi ambalo alienda kwenye ofisi zake kuelezea
anavyojutia uamuzi huo uliomgharimu.
“Wasanii wengi ni wabunifu na hufanya mambo kwa nia ya kufurahisha
mashabiki kama ambavyo amekuwa akifanya Joti kuvaa nguo za kike na
kupaka rangi ya mdomo, hivyo mavazi yangu yalikuwa na lengo la kutoka
tofauti mbele za mashabiki wangu, lakini kwa yaliyonikuta hasa kwenye
vazi la Kili niliomba msamaha kwa jamii na bado naomba wanisamehe,”
alisema Faiza huku akidaiwa kububujikwa na machozi.
“Hakika nimejikuta kwenye wakati mgumu na sivyo ambavyo baadhi ya watu
wanafikiri. Hali hiyo ilinitokea nikiwa kule kule kwenye Kilimanjaro
Music Award tena baada ya kubaini picha zinazoonyesha makalio yangu
zimewekwa kwenye mitandao. Niliamua kuondoka haraka katika eneo hilo,
kabla ya muda niliyokusudia,” aliliambia Mwananchi.
“Ingawa nimezoea kuvaa nguo fupi lakini sikupanga kuonyesha makalio,
bahati mbaya ni kwamba ile nguo nilipoivaa awali kabla ya kuondoka
nyumbani ilikuwa imekaa vyema. Nafikiri baada ya kukaa kwenye gari
ilifumuka bila mimi kujua, hadi nafika ukumbini na kuingia pale kwenye
zulia jekundu natembea kumbe huko nyuma mapaparazi wanapiga picha.
Hakuna hata aliyenishtua. Napenda kuweka wazi naumizwa na watu ambao
wanaendelea kusambaza hizo picha za makalio, watambue tu leo imenifika
mimi lakini siku nyingine itawafika na wao maana sisi sote ni binadamu,
tunafanya makosa kwa nyakati tofauti.”
“Namshukuru Mungu nimeweza kuhimili hali hii kwa kiasi fulani, maana
naamini mtu mwingine angeweza hata kuamua kuwa mlevi au kuwa mbaya
lakini nashukuru nina uamuzi wa kubadilika, nampenda mwanangu sitaki
kuwa mbali naye
No comments:
Post a Comment