kwa mujibu wa data
zilizochapishwa na taasisi ya CIES Football Observatory, mshambuliaji
wa Barcelona, Lionel Messi kwasasa ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa
zaidi kwenye soko la uhamisho, akifuatiwa na nyota wa Chelsea, Eden
Hazard, halafu straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anashika nafasi
ya tatu.
Namna gani CIES Football Observatory wamepata matokeo hayo?
Ili kupiga hesabu ya thamani ya uhamisho wa mchezaji yeyote, wametumia sababu mbalimbali za kisoka.
Sababu hizo ni pamoja na Umri wa mchezaji, mkataba wake wa
sasa, nafasi anayocheza uwanjani, jumlisha matokea na mafanikio ya klabu
yake.
Hapo chini ni graphics zinazoonesha sababu za kupata thamani ya uhamisho wa mchezaji:
Matokeo ya utafiti wao yanaonesha kuwa Lionel Messi ndiye
mchezaji mwenye thamani kuwa zaidi kwenye soko la uhamisho akiwa na bei
ya Euro milioni 255.3-280.8.
Mchezaji wa Chelsea, Eden Hazard ameshika nafasi ya pili akiwa na thamani ya Euro milioni 135.4-148.9.
Cristiano Ronaldo, ameshika namba tatu akiwa na thamani ya Euro milioni 113.3-124.7.
Ukiachana na Ronaldo ambaye
amefikisha miaka 30, wachezaji sita tu wenye umri huo wameingia kwenye
orodha ya wachezaji 100 ambao ni Yaya Toure, Santi Cazorla, Andrés
Iniesta, Carlos Tevez, Thiago Silva na Luiz Fernandinho.
Matokeo hayo pia yanaonesha,
Raheem Sterling wa Liverpool ameshika namba sita kwa kuwa na thamani
kubwa kwenye soka la uhamisho, wakati mshambuliaji wa Tottenham, Harry
Kane anashika nafasi ya 15.
Tazama Orodha nzima hapo chini:
No comments:
Post a Comment