MAISHA haya siku hizi balaa tupu! Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kwembe, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam (jina limefichwa), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Magomeni kwa madai ya kumchoma kisu dereva wa daladala.
Uwazi limenasa mkasa huo uliotokea Juni Mosi, mwaka huu eneo la Manzese na kubaini kuwa aliyechomwa kisu hicho kifuani ni Dotto Madaraka (35) anayeendesha daladala lenye namba za usajili T 241 DDF linalomilikiwa na Kampuni ya Torabora Trans, linalofanya safari zake kati ya Mbezi ya Kimara na Kivukoni, Dar.
“Basi lilikuwa limebeba wanafunzi wengi na abiria wengine, tulipofika eneo la Manzese mtuhumiwa alianza kugombana na mwanafunzi mwenzake wa kike, ugomvi ambao haukujulikana chanzo chake.
“Kifupi waligeuka kero, kondakta wa daladala akaona ili kumaliza vurugu kwenye chombo chake cha usafiri ni vema amshushe mtuhumiwa pale Manzese ili apande gari jingine,” mmoja wa abiria wa gari hilo ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini, aliliambia Uwazi.
BONYEZA KUISMO YOTE===>>

No comments:
Post a Comment