Christian Bella aka King of the best melodies amedai kuwa kazi yake
mpya na Alikiba itakuwa na utofauti mkubwa kwakuwa Kiba amebadilisha
kwenye wimbo huo.
Alikiba, Bella pamoja na Aidan wakiwa ndani ya studio
Akizungumza na Bongo5 leo, Bella amesema Kiba ni msanii aliyeweza kwenda naye sambamba kwenye kupanda na kushuka kwa sauti.
“Nimefurahi jinsi tulivyoelewana masauti humu ndani,” amesema Bella.
“Nimemfanya sasa Alikiba kuimba na mimi akaonyesha kiwango kingine
baada ya kukaa na king of the best melodies. Nilinyoosha melody na yeye
ikabidi atembee vile vile, njia niliyopita mimi pick za juu sana na yeye
akapita humo humo pia. Yaani imekuwa nzuri sana yaani kinoma. Kwahiyo
ngoma ipo tayari,” ameongeza.
Hata hivyo muimbaji huyo amesema bado wimbo huo haujapewa jina.
“Jina na wimbo bado halijakamilika lakini baada ya leo ndo tutajua unaitwaje,” amesisitiza Bella.
“Sasa hivi tunajipanga kuhusu video na video ikikamilika baada ya
mwezi wa ramadhani ngoma itatoka. Sitapenda ichelewe kwa sababu
mashabiki walikuwa wanasumbua tufanye kolabo na Alikiba na ndo umefika
muda wao kupata kile walichohitaji. Ingawa imechukua muda kutokana na
sisi sote kuwa busy, kwahiyo mipango iliyobaki ni video ili tutoe video
pamoja na audio na video tutafanya video kubwa kwa ufupi tu na sidhani
kama tutashoot hapa nchini.”
alimalizia Bella
No comments:
Post a Comment