27 May 2015

Yanga SC yamleta Samatta Dar


Yanga hadi sasa wamefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Deus Kaseke huku ikiwabakiza Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Deogratius Munishi ‘Dida’ ambao ilikuwa ikidaiwa kuwa wanaweza kutimka.MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wanatarajiwa kuwaleta mabingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), Kaizer Chiefs, pamoja na TP Mazembe wanaocheza Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa ajili ya kuwapima nyota wao wapya waliowasajili.
Timu hiyo, bado inaendelea na usajili na hivi sasa inawania saini ya mshambuliaji wa Platinum FC ya Zimbabwe, Donald Ngoma, Haruna Chanongo wa Simba na Salum Mbonde wa Mtibwa Sugar.

Akizungumza na Championi Jumatano, ofisa habari wa timu hiyo, Jerry Muro, alisema kuwa wamepeleka barua za mialiko kwenye klabu mbalimbali zitakazofika kusherehekea sherehe yao ya ‘Yanga Day’ itakayofanyika Juni 15, mwaka huu.
Muro alisema, tofauti na Kaizer Chiefs wamezialika Zesco ya Zambia na TP Mazembe ya akina Samatta.
Aliongeza kuwa kwa upande wao siku hiyo ya sherehe wamepanga wacheze na Kaizer Chiefs huku TP Mazembe na Zesco zikipambana zenyewe

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname