26 May 2015

VITA DHIDI YA DIAMOND NI KUBWA KULIKO TUNAVYOFIKIRIA,

Hakuna ubishi kua kwa sasa diamond platnumz ndie msanii anae ongoza kupigwa vita kuliko msanii yeyote hapa nchini.
Vita hiyo ina ongozwa na baadhi ya walio wahi kuwa wapenzi wake pia na mahasimu wake wa kimuziki (wasanii wengine) kupitia mashabiki zao.
Sawa ni jambo la kawaida kwa wasanii wakubwa duniani na mastar wengine kama wachezaji,maboxer pamoja na waigizaji kuwa na maadui hili linathibitishwa na mfano wasanii kadhaa wa kimarekani walivyo na maadui mpaka inafikia kupigana risasi mfano 2pac,BIG,50cent,mayweather na wengine kibao.

Sababu kubwa za diamond kuanzishiwa vita "maalum" ili ashuke kimuziki na kimafanikio ni kutokana na maneno ya wengi eti kua anaringa,anadharau,ana nyodo,ana mamneno ya shombo,ana ropoka sana,mtoto wa uswahili,hajasoma,mchawi na visababu kedekede.
Wadadisi wa mambo wanasema kua chuki dhidi ya diamond si tu inatokana na sababu zilizo tajwa hapo juu bali inaenda mbali zaidi mapaka kwa team nzima ya diamond hasa mameneja wake.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname