Shindano la Fanya Kweli Kiwanjani limeanza kutimua vumbi kwa kuzishindanisha baa mbalimbali za jiji la Dar es salaam kama ilivyokua imetangazwa hapo awali.
Mapema
jioni ya jana, wadhamini wanaoendesha shindano hilo Kampuni ya Bia ya Serengeti
kupitia bia yake cha Tusker Lager wakishirikiana na kituo cha redio E-fm,
walifunga kambi katika baa hiyo iliyopo Kimara-Korogwe jijini Dar na
kuporomosha burudani ya nguvu huku wakitoa zawadi mbalimbali kwa wapenzi wa
kinywaji cha Tusker waliojumuika kwenye hafla hiyo.
Kikubwa
kilichowavutia zaidi wateja waliofika kwenye baa hiyo ni huduma nzuri ya
vinywaji, vyakula, fursa ya kutuma salamu moja kwa moja kupitia redio E-fm
sambamba na zawadi kutoka SBL kama Tisheti na bia za bure za Tusker
zilizotolewa kwa wateja hao na mtangazaji wa E-fm Bw. Gadner kwa staili mpya
iliyojulikana kama Mupe Mureke.
Mmoja
kati ya wateja wa baa hiyo aliyejishindia Tisheti na bia za bure katika hafla hiyo
kwa jina la Wema Usiri (30) akizungumzia baa hiyo alisema… “Nimefurahi sana
baada ya kusikia “Toroka uje” imekua baa ya kwanza kushinda promosheni hii ya
Fanyakweli Kiwanjani kiukweli inastahili”. Bi Usiri aliongeza kuwa sababu kubwa
inayoifanya baa hiyo kupendwa sana ni kutokana na huduma zao nzuri hasa upande
wa vyakula, vinywaji sambamba na burudani za kila aina kama muziki wa bendi
unaopigwa kila ijumaa na jumamosi mahali hapo. Wengine walioibuka na zawadi za
bia na Tisheti ni Bwana na Bi Lema, Romana Mwikombe na Anneth Kimaro.
Kwa
upande wake Meneja Vipoozeo na mwonekano wa Kampuni ya Bia ya
Serengeti Bw. Baraka
Mandara aliyemwakilisha Meneja Chapa wa Tusker alianza kwa kuwashukuru wananchi
wa Kimara-Korogwe na wapenzi wote wa Kinywaji cha Tusker waliofika kwenye hafla
hiyo ili kusherehekea kwa pamoja ushindi wa baa hiyo. “Lengo kuu la Kampeni hii
ni kuziwezesha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli kwa
kuzitambulisha kwa wananchi ambao tunaamini kutokana na sapoti yao baa hizi
zitaongeza vipato.”
Bw.
Mandara aliendelea kwa kusema kuwa “Toroka uje” ndio baa ya kwanza kufungua
promosheni hiyo na kuwasisitiza wapenzi wa Kinywaji cha Tusker kuendelea kupiga
kura kwa wingi ili kuziwezesha baa za mitaa yao kushinda.
Promosheni
hii ya “FanyaKweli Kiwanjani” ni muendelezo wa Kampeni ya Tusker
“FanyaKweli” ambapo itadumu kwa takriban muda wa wiki tano huku zaidi ya
baa 50 za jiji la Dar es salaam zikipewa fursa ya kushiriki kwenye shindano
hilo. Kila wiki kutakua na mshindi mmoja kati ya baa 10 zitazokuwa kwenye
kinyang’anyiro. Ili kuiwezesha baa ya mtaa unaoishi tembelea baa hiyo kisha
burudika na kinywaji cha Tusker na piga picha nyingi uwezavyo na uipendekeze
baa hiyo kwa kuweka picha hizo kwenye kurasa za jamii (Facebook na Twitter) za
Tusker au kusikiliza kipindi cha ubaoni kinachorushwa na redio E-fm kati ya saa
tisa hadi moja usiku ndani ya siku za juma kwa maelezo zaidi.
-MWISHO-
No comments:
Post a Comment