01 May 2015

TANESCO WAVUNJA MKATABA NA SELCOM ...KUTOKANA NA TATIZO LA LUKU

Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuifutia kazi Kampuni ya Selcom kwa kushindwa kutoa huduma bora ya mfumo wa Luku.
Kutokana na mitambo yao kutokidhi vigezo na kusababisha usumbufu kwa jamii baina ya watumiaji wa umeme wanaonunua umeme kwa njia ya kielektronikia. Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunja mkataba kati yao na kampuni hiyo ya Selcom, kutokana na kero kubwa inayoletwa na kampuni hiyo na watumiaji wa umeme kushindwa kununua umeme kwa ya kielektronikia.
Kwa muda zaidi ya siku mbili umeme umeshindikana kununulika kwa mitandao ya simu na mashine za Selcom, ambao ndio mawakala wakubwa wa kampuni hiyo ya Tanesco kwa kusambaza luku nchi nzima na kusababisha watu kishinda kiza na baadhi ya biashara kutofanyika kutokana na kukosekana kwa umeme.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname