Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa na mwanaye.
SIKU chache baada ya
kuripotiwa na gazeti pacha la hili, Risasi Jumamosi kuwa staa wa sinema
za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alibeba mimba na kuzaa kwa siri
huku tetesi zikivuma kuwa baba wa mtoto huyo ni msanii mwenzake, Vincent
Kigosi ‘Ray’, mambo yameanza kunoga baada ya Ray kufunguka kuwa
hahusiki kwa lolote, Risasi Mchanganyiko ‘limemzingira’.
Staa wa filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’.
Hivi karibuni gazeti
hili lilimbana staa huyo anayetamba sokoni kwa sasa na Filamu ya Chicken
Head baada ya kubambwa nje ya Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini
Dar, kulikokuwa na sherehe za Tuzo za TAFA ambapo aliweka wazi.
Awali, Ray alisema si busara wala hataki...
kuzungumza mengi juu ya
madai hayo kwani hahusiki kwa lolote na kwamba watu wasimtafsiri
kutokana na maneno yasiyokuwa na ukweli huku akimtaja mpenzi wake wa
sasa, Chuchu Hans kuwa ndiye mwanamke wake wa maisha.
Ray alifunguka kuwa,
kati ya mambo yanayomchukiza ni ama kuzushiwa au kuhusishwa na mambo
ambayo yanamfanya aonekane wa hovyo katika jamii na kusisitiza kusiwepo
na mjadala unaopingana na kauli zake.
Huku akiwa amemganda
Chuchu kimahaba mbele ya kadamnasi, Ray alikwenda mbele zaidi na kusema
ni jambo la heri kujiweka mbali na watu wanaotafuta umaarufu kupitia
migongo ya watu, kauli iliyozua viulizo kwa waandishi wetu na yeye
kushindwa kuifafanua kwa kile alichokiita ‘hakuwa na mudi ya mazungumzo
zaidi’.
“Achaneni na hayo mambo,
sihusiki kwa lolote na jambo hilo (mtoto) na sipendi kabisa kuzushiwa
mambo kama hayo, watu wasinitafsiri kwa minong’ono na badala yake
wafuate ninachokisema.
“Kwa sasa mwanamke wa
maisha yangu ni huyu (Chuchu) na nitakuwa natembea naye kila mahali ili
kuwafunga midomo wanaojinadi kuwa ni wapenzi wangu,” alisema Ray huku
akiwatazama waandishi wetu kwa macho ya ‘nadhani mmenielewa sasa’ na
kuondoka eneo hilo sanjari na mahabuba wake.
Hivi karibuni Johari
alithibitisha kuwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miezi saba ambaye
alimpa jina la Maria linalofanana na la mama wa Ray hivyo kuibua
minong’ono kuwa huenda jamaa huyo anahusika.
No comments:
Post a Comment