13 May 2015

Ngassa asaini miaka 4 FREE STATE, Alamba $80,000,Mshahara $5,600, Nyumba Gari Bure

 
Mrisho Ngassa ametua zake Free State Star ya Afrika Kusini na kupokelewa kwa shangwe.

Mmoja wa waliompokea ndani ya aneo la Bethlehem ni Kocha Kina Phiri, mshambuliaji wa zamani nyota wa Malawi
Ngassa amejiunga na Free State Star akitokea Yanga ambayo ameichezea kwa mafanikio makubwa.

Ngassa ameiambia SALEHJEMBE kutoka Afrika Kusini kuwa mambo yanakwenda vizuri.


“Lakini ningependa nimalize mambo kadhaa muhimu hapa halafu tutazungumza,” alisema mtoto huyo wa mshambuliaji nyota wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba, Khalfan Ngassa

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname