21 May 2015
Miss mwenye asili ya rangi nyeusi kupambana na Ubaguzi wa rangi Japan
Kwa mara ya kwanza tangu Japan ianzishe mashindano ya Mlimbwende (Miss) miaka kadhaa iliyopita, hatimaye mwaka huu amepatikana Miss mwenye asili ya rangi nyeusi.
Mlimbwende huyo anaetambulika kwa jina la Ariana Miyamoto, mwenye umri wa miaka 21, Mama yake ni mjapani na Baba ni mtu mweusi kutoka Amerika amesema atahakikisha anapambana na tatizo la ubaguzi wa rangi kwenye fani ya ulimbwende nchini Japan.
Wakati akifanya mahojiano na gazeti la AFP Ariana Miyamoto, amesema, “Wakati naingia kwenye fani hii nilijiandaa kupokea changamoto haswa zile za kutokukubalika na wajapani wenye rangi nyeupe ndio maana pamoja na maneno yanayosemwa kwenyemitandao ya kijamii kwamba sijastahili kupata huu ushindi hata sitishiki ”.
Ariana Miyamoto amemalizia kwa kusema nia yake ni kupambana kutokomeza kabisa tatizo la ubaguzi mwisho wa siku hata wajapan wenye asili ya rangi nyeusi waheshimike kwenye fani ya ulimbwende na mitindo nchini Japan
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment