This is a love and hate type of sh*t. Wema Sepetu amekiri kuwa upande
wa Alikiba lakini bado anazipenda nyimbo za mpenzi wake wa zamani,
Diamond.
Unakipata kizungumkuti cha kauli hiyo sio? Hivi karibuni Wema
alitengeneza vichwa vya habari kwa kuonesha support kubwa kwa Alikiba
(hasimu wa Diamond) katika kumuombea kura za KTMA. Kwa wengi hiyo
ilitafsiriwa kama kisasi cha Wema kwa ex wake. Na wengine walihisi Kiba
na Wema wana lao jambo! Lipi?
Hata hivyo kupitia kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Jumatatu
hii, Wema alisema Kiba ni mtu wake wa karibu tangu siku nyingi na
humuita jina la utani ‘bichwa’.
“Ali and I are very good friends,” alisema Wema. “Ali alinitumia
meseji kwenye whatsapp akanitumia picha (za KTMA) kama nne, nikamuambia
ipi? Akaniambia zote, nikapost zote, akaniambia ntakutumia zingine.
Nikamuuliza ‘hivi umetajwa kwenye category ngapi kwenye Kili? Akaniambia
saba. Nikamwambia fresh nitumie zote nitakupost. Akaniambia poa na wewe
nitumie post zako za Tuzo za watu and I took it as a support,
namsupport mshkaji wangu. Mimi ni team Kiba.”
Hata hivyo Wema alisema haoni kama kuna tatizo kama akiwa team Diamond pia.
“I love his [Diamond] music. Mtu akikaa leo akisema kwamba Diamond
anaimba vibaya huyo atakuwa ni hater tu, the boy can really sing.”
No comments:
Post a Comment