LULU |
Sheria iliyopitishwa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA "Cybercrime
au Cyberbulling" Kuwa ukitumia lugha chafu mtandaoni na Comment ikawa
inaonekana aliyeandika utalipa faini ya Shiling laki 7.5 kwa kila siku
imemfanya Lulu Michael Arudi Mtandaoni Baaada ya Kujitoa kutokana na
Matusi ya Watu waliokuwa wakimshambulia . Lulu Amesema "Binafsi nadhani
Sheria hii Itasaidia Kidogo Watanzania kupunguza matumizi Mabovu ya
Mitandao ya Kijamii , Fikiria wazazi wetu wangetulia kwa kutukana kama
ilivyo sasa tungekuwa wapi sasa hivi? "
Huku Lulu Akishangalia Sheria Hiyo Mrembo Wema Sepetu Amepinga Vikali Sheria hiyo kwa kusema inanyima uhuru kwa Mashabiki wake kumrekebisha , Wema Amesema yeye yuko radhi kutukanwa kwani ndio kunamrekebisha ......"Je mimi nitawezaje kujua makosa yangu ili niweze kubadilika na kufanya vizuri kama sintasikiliza maoni ya watu yawe mabaya au Mazuri" Ali hoji Wema Sepetu.
No comments:
Post a Comment