Familia
inayoundwa na wanandoa Bianca na Nick Bowser, ni familia yenye furaha
lakini iliyowashangaza wengi baada ya Nick ( baba wa familia) kupata
ujauzito na kujifungua.
Iko
hivi; Nick ambaye ana umri wa miaka 27 hivi sasa, alizaliwa na jinsia
ya kike na kupewa jina la Nicole na wazazi wake, lakini aliamua
kubadilika na kuishi kama mwanaume (transgender/jike dume) tangu miaka
saba iliyopita. Na hii ilichangiwa pia na sura na umbo la kiume
alilokuwa nalo.
Hali
ilikuwa hivyo pia kwa Bianca ambaye ana umri wa miaka 32 hivi sasa,
yeye alizaliwa mwanaume na kuitwa jina la Jason, lakini kutokana na kuwa
na sura nzuri na umbo la kike, na hisia zake za kutaka kuishi kama
mwanamke, alibadili aina ya maisha na kuishi kama mwanamke kamili.
Wawili
hao walikutana na kuamua kufunga ndoa huku wakiyabadilisha kabisa
maisha ya wana ndoa, Nick akiwa baba wa familia anaevaa na kuishi kama
mwanaume. Mkewe Bianca (ambaye ni mwanaume) yeye alibadili na kuishi
kama mwanamke kamili akiihudumia familia yake na kuvaa mavazi ya kike
kama mama siku zote
.BOFYA HAPA KUMWONA AKIWA NA FAMILIA YAKE
.BOFYA HAPA KUMWONA AKIWA NA FAMILIA YAKE

No comments:
Post a Comment