20 April 2015

Rais atuhumiwa kutaifisha gari la shirikisho la filamu



Rais wa shirikisho la filamu nchini, Tanzania Film Federation (TAFF), Simon Mwakifwamba amepinga tuhuma zinazomkabili za kutaifisha gari la shirikisho hilo na kulifanya kua mali yake binafsi.
Habari zimezagaa mtaani kwamba Mwakifwamba amebadili kadi ya gari la Shirikisho na kuandika jina lake huku akilitumia kwa shughuli zake binafsi.
Akizungumza wakati wa mahojiano wa njia ya simu kwenye kipindi cha Filamunata cha Radio Times Fm kinachokwenda hewani kila siku ya jumapili saa tano mpaka saba mchana. Mwakifwamba amesema habari hizo si za kweli huku akisisitiza gari hilo bado ni mali ya Shirikisho.
Kumekua na mvutano na mvurugano ndani ya shirikisho la filamu kwa muda sasa hatua ambayo imepelekea kufukuzwa kwa katibu wa shirikisho hilo ndugu Bishop Hiluka baada ya kupigiwa kura ya kutoaminiwa.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname