19 April 2015

MWANAMKE AKIRI KUANZISHA DANGURO LA WASICHANA

 Ni biashara ya ngono ikiwamo ya jinsia moja ,Wasichana wazungumza suluba wanazopata

Mwanamke mmoja, mkazi wa Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, anadaiwa kuanzisha danguro la wasichana na kuendesha biashara ya ngono ikiwamo ya jinsia moja.Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la mama Uzuri, anadaiwa kuwachukua wasichana hao kutoka vijijini kwa kuwadanganya kuwa anakwenda kuwatafutia kazi mjini Inadaiwa kuwa fedha anazopata kutokana na biashara hiyo, huzitumia kama gharama ya kuwatunza wasichana hao.Wakizungumza Jumapili kwa nyakati tofauti, wasichana hao (majina yanahifadhiwa), walidai kuwa mwanamke huyo aliwachukua vijijini kwao kwa ahadi ya ajira za ndani.
Wakielezea undani wa biashara hiyo, walisema wanaume wengi wamekuwa wakiwalazimisha kufanya mapenzi bila kinga (kondom), kwa madai kuwa kwa kufanya hivyo kunawanyima starehe ya tendo hilo.
Suzana (sio jina lake halisi), alisema makazi yao ni nyumbani kwa mwanamke huyo ambapo hulelewa katika mazingira mazuri, na kati yao kuna makahaba na wasagaji.
Alisema, mwanzo walipoanza biashara hiyo walipata wakati mgumu lakini kadiri siku zinavyokwenda waliizoea.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname