23 April 2015

MJENGO WA DIAMOND PLATINUMZ NI MAJANGAZ

Akizungumza na Gazeti la Amani mwanzoni mwa wiki hii baada ya nyota huyo kutupia picha za uzio wake katika mtandao ukiwa chini kwa mwereka wa mvua, Injinia Stuart alisema anaamini nyumba ya Diamond imejengwa chini ya kiwango na mafundi walimchakachua simenti.
SIKU chache baada ya sehemu ya ukuta wa uzio wa mjengo wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuanguka, mtaalam wa majengo aliyejitambulisha kwa jina la Injinia Stuart Daniel ameupiga zengwe akidai licha ya kuonekana kuwa na nakshinakshi nyingi, lakini ni dhaifu na unaweza kudondoka.

“Kama jengo lote lilijengwa kwa staili hii, basi ni suala la kusubiri kwa muda tu kabla hatujasikia habari za kuanguka kwake na kama hatakuwa makini, linaweza kumletea madhara makubwa. “Kitu ambacho ningeweza kumshauri ni kuwaita wakaguzi wa majengo waangalie mafundi wake walivyojenga ili kuepuka hasara anayoweza kuipata,” alisema mtaalam huyo.” SOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname