Mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) amemshambulia kwa maneno makali hasimu wake na adui namba moja
wa Chama chake Mhe Zitto Kabwe kwa kumuita muongo na kwamba amewatumia
waandishi wa Habari kuandika taarifa za Uzushi kuhusu Mnyika.
Mnyika ametoa tuhuma hizo dhidi ya Zitto asubuhi hii kupitia akaunti
yake ya Twitter na kumtahadharisha Zitto kuwa atamchukulia hatua Kali za
kisheria kwa kupitosha mazungumzo ya Mnyika na familia ya Mwalimu
Nyerere.
Sasa hivi imebainika kuwa ni vita kamili baina ya Zitto na Mnyika hasa
baada ya kubainika tetesi kuwa Zitto anagombea jimbo la Ubungo ambalo
liko chini ya Mnyika hivi sasa.


No comments:
Post a Comment