12 April 2015

HAWA NDIO WASANII WATAKAOGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHADEMA

Hii tabia ya CHADEMA kutumia wasanii wa bongo fleva & movie kisiasa ni upunguani wa hali ya juu sana.

Iweje leo hii kisa tu chama kinataka ruzuku ya kutosha kione ni vyema na sawa kuokota tu vijana wasio kuwa na maadili kutoka kwenye tasnia za muziki na movie na kuwanadi ili wawakilishe wananchi bungeni!? Huu ni wehu na kukosa kufikiri!
CHADEMA wamezindua mpango uitwao "Kujaa bungeni kivyovyote" na haya ya kujaza wasanii ndio mkakati wa kufanikisha mpango huo!
Kwa taarifa sahihi kutoka CHADEMA makao makuu, wafuatao wanatarajiwa kusimamishwa na CHADEMA kwenye majimbo ya uchaguzi oct mwaka huu:
1) Irine Uwoya - Jimbo la Mtera
2) Prof Jay - Jimbo la Mikumi
3) JB (bongo movie) - jimbo la Kigamboni
4) Sugu - Jimbo la Mbeya Mjini
5) Juma Nature - Jimbo la Temeke
6) Dully Sykes - Jimbo la Ilala
7) Fid Q - Jimbo la Magu

Je, wewe Mtanzania una kubaliana na hawa CHADEMA kukupa wawakilishi wa aina hii? Maana CUF na NCCR hawana kauli huku bara ya kupanga wagombea wanaojitambua na kujua wajibu wao kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname