Esma
mdogo wa Diamond Platnumz, aliyevunja ukimya, asubuhi ya leo juu ya
kufuatwa fuatwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wa marafiki wa Wema Sepetu
#teamWema, ambao wamekuwa wakitukana na kumtaka asimsaidie kaka yake juu
ya shughuli zake za muziki.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Kuna
misemo mingi juu ya mawifi wengi ‘wanagugu’ hasa wa ndugu wa mme, hilo
ndilo lililomkuta dada wa mwanamuziki nyota nayefanya vizuri Bongo nan
je ya Bongo, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ ajulikanaye kwa jina la Esma
maalufu kama ‘Esma Platnumz’ ameamua kufunguka kufuatia kusemwa semwa
sana na jamaa wa mmewe, ambao ni kutoka #teamWema.
Esma
ambaye ameolewa na Meneja wa msanii Mirror na mfanyakazi wa kampuni ya
Wema Sepetu, Endless Fame Films aitwaye Petit Man, ambapo kupitia
ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, mapema asubuhi ya leo aliamua
kufunguka juu ya wanaomfuatafuata kwa kile anachokiposti hasa
kinachohusiana na ‘issue’ za Diamond Platnumz ikiwemo shoo yao ya Mei
Mosi mwaka huu, Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment