Mkitaka
kujua afya yangu, mimi ni mzima, namshukuru Mungu naendelea
kutimiza majukumu yangu, likiwemo hili la kuwaandikia barua.
Nimewakumbuka
leo kupitia barua, nataka kuwaambia kwamba mimi pamoja na mashabiki
wengine wa sanaa yenu tumewachoka. Tumechoka kuona na kusikia kila
siku mkifanya maigizo kwenye maisha yenu halisi.
Hivi ni kwa nini
kila kukicha tunasikia mnaachana? Kwa nini hamdumu kwenye uhusiano wa
mapenzi? Kwa nini hamdumu kwenye ndoa kama mashabiki wenu
wanavyowategemea?
Penzi linapoanza kushamiri, mnalinadi kwenye
mitandao na vyombo vya habari. Mnawaaminisha mashabiki wenu kuwa
mnapendana kwa kauli zenu motomoto lakini ndani ya miezi miwili mitatu
penzi chali.Wengine mnaonesha kwamba mmedhamiria na kuamua kufunga
ndoa kabisa, lakini kumbe moyoni bado mnakuwa mna lenu jambo.
Mashabiki wenu wanafurahia kuona mmeoana lakini ndoa nayo haidumu,
mnaachana.BOFYA KUISOMA YOTE>>
No comments:
Post a Comment