11 March 2015

Wema Awa Mbogo Kisa Kutajiwa Diamond


Vijimambo:Mrembo na staa wa Bongo Movie asiyekaukiwa na visa na mikasa, Wema Sepetu amezua kioja cha aina yake baada ya kutajiwa jina la aliyekuwa mwandani wake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kioja hicho alikifanya juzikati nyumbani kwake, Kijitonyama jiji Dar alipokuwa akirekodi kipindi chake cha In My Shoes ndipo aliposhtuka baada kutumiwa maoni na moja wa shabiki wake kupitia mtandao wa simu.“Heeeh! Huyu vipi tena ananitajia jina hili (Diamond)? Sitaki kabisa kulisikia, hapa nataka kusikia mimi na maisha yangu na si maisha ya mtu mwingine,” alisikika Wema.
GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname