13 March 2015

MOZA MBARONI KWA KUMDHALISHA SUPER STAR EZDEN LIVE


JESHI la polisi jijini Dar limemkamata binti anayefahamika kwa jina la Moza kwa kosa la kudaiwa kumdhalilisha Mtangazaji wa Runinga ya TV1, Ezden Jumanne ambapo anatarajiwa kuburuzwa mahakamani muda wowote baada ya uchunguzi kukamilika.
Moza anayedaiwa kumrekodi Ezden video ya utupu.

Moza ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji huyo kisha kuachwa, anadaiwa kumrekodi video ya utupu Ezden kipindi walipokuwa kwenye uhusiano mzuri kisha kuisambaza mitandaoni walipogombana.

Chanzo makini kimedai kuwa, Moza alikamatwa na kuwekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar kufuatia msako mdogo uliofanywa na polisi saa chache baada ya mrembo huyo kuvujisha video hiyo.
“Wameshamtaiti pale Oysterbay, wanakamilisha tu taratibu za ushahidi kisha anaburuzwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa,” kilisema chanzo chetu, juzi Jumatano. Moza amedaiwa kuiachia video hiyo mapema wiki hii kutokana na chuki za kuona Ezden ana mwanamke mwingine hivyo akaona akivujisha video hiyo atakuwa amemkomoa mtangazaji huyo kijana aliyewahi kuwa mume wa Mtangazaji Khadija Shaibu ‘Dida’.

Mtangazaji wa Runinga ya TV1, Ezden Jumanne. Akizungumzia sakata hilo, Ezden alisema yeye ni mtu anayejiheshimu, anajitambua hivyo kitendo cha mwanamke huyo kumrekodi video hiyo hakikuwa cha kiungwana.
“Hakunitendea haki, Nimeshalifikisha suala hili polisi, taratibu za kipolisi zikikamilika anaburuzwa mahakamani,” alisema Edzen.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname