Kocha Marsh alifariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akitokea Mwanza baada ya hali yake kuwa mbaya.
Mamia ya watu wakiwemo viongozi wa kiserikali, wadau wa soka, wanasoka na mashabiki wamehudhuria mazishi hayo yaliyoanzia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Milongo ambapo marehemu Marsh na vijana wake walikuwa wakifanyia mazoezi.
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu lilianza asubuhi katika uwanja huo baada ya mwili kuwasili kutoka katika Hospitali ya Seketule ulipokuwa umehifadhiwa.
Vijana waliokuwa wakifundishwa na Marsh katika Kituo cha soka cha Marsh Academy ndiyo waliopewa jukumu la kubeba jeneza la mwalimu wao.
Wanasoka wa zamani akiwemo Edibily Jonas Lunyamila na Fumo Felician ambao waliwahi kucheza soka na marehemu kabla ya kuwa kocha walimwaga machozi wakati wa zoezi la kumuaga mwenzao.
Wasanii wakiwemo Steve Nyerere na H-Baba nao wameungana na waombolezaji kumuaga mwalimu Marsh.
Sylvestre Marsh aliyezaliwa miaka 55 iliyopita, licha ya kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars tangu enzi za Marcio Maximo hadi Kim Poulsen, pia aliwahi kuwa kocha wa timu kadhaa zikiwemo Azam FC na Kagera Sugar.
(PICHA ZOTE NA JOHNSON JAMES / GPL, MWANZ
No comments:
Post a Comment