Kumekuwa na story ambayo imeenea sana mitandao ya kijamii na pia watu
wamekuwa wakitumiana PICHA Whatsapp na wengine wameweka pia kwenye
kurasa za Instagram na kuandika #RIP picha ya mchekeshaji wa kundi la
Orijino Komedi, Joseph Shamba aka Vengu ambaye ni muda mrefu hatujamuona
akiigiza pamoja na kundi lake kutokana na kuumwa.
Taarifa ambayo Clouds FM imeipata baada ya kuwasiliana na Seki pamoja na
Joti ni kwamba hakuna ukweli wowote kuhusu taarifa za msanii huyo
kufariki.
“Kuna taarifa zilizosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa
muigizaji wa vichekesho #Vengu kafariki dunia.. Kwa mujibu wa Meneja
wake #Seki na muigizaji mwenzake #Joti wamekanusha taarifa hizo na
kusema yuko hai..“–@cloudsfmtz
-Millard Ayo
No comments:
Post a Comment