Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT
GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi chaKati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojianokuhusu tuhuma za kashfa na matusi.Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama KaldinariPolycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitiamitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sautiiliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu
Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali
ambayo pia imewaudhi watu wengine.
Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali
ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe
sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya
Dar es Salaam bila kukosa.
No comments:
Post a Comment