Kikao cha Rais na watu wenye ulemavu wa ngozi Albinism almanusura
kivunjike baada ya walemavu hao kuhamishia mgogoro wao wa uongozi ikulu
na kusababisha vurugu iliyopelekea watolewe nje ya jengo la ikulu na
baadae kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe.
Mapema asubuhi walemavu hao walifika eneo la mapokezi ikulu ambapo
waliokuwa wameorodheshwa kwa ajili ya kuonana na rais waliahikiwa majina
yao lakini likajitokeza kundi lingine ambalo halikuwa kwenye orodha
muda wa waliotakiwa kuingia ndani ulipowadia ndipo vurugu zikaanza za
kuwazuia viongozi hao wasiingie ndani bila wao kwa madai kuwa kwa sasa
hawana viongozi.
Tafrani hiyo iliendelea kwa muda na kusabisha shughuli zote za
mapokezi kusimama kutokana na kelele zilizosababishwa na walemavu hao
hali iliyosababisha askari waliokuwa eneo hilo kuingilia kati na kuanza
kuwasihi watoke nje ya geti wakajipange upya huku baadhi yao wakieleza
kusikitishwa na kitendo hicho na kwamba kimewatia aibu.
Mara baada ya kutoka nje ya geti la ikulu walianza kurushiana
maneno wao kwa wao na waandishi wa habari walipotaka kuzungumza na
mwenyekiti waliyemkataa kwa madai kuwa uongozi wake uliisha mwishoni mwa
mwaka jana kundi hilo lilitokea tena na kuanza kumzomea hali
iliyosababisha ashindwe kuendelea na mahojiano na hapo ndipo ngumi
zikaanza.
Maafisa usalama walifanikiwa kumuokoa mwenyekiti huyo ambapo baada
vurugu kutulia askari aliyevalia sare alisikika akiwasihi walemavu hao
kuondoka eneo hilo kwa amani huku baadhi yao wakielezea sababu za
kuwazuia viongozi hao kwenda kuonana na rais.
Hata hivyo baada ya kundi hilo kuondoka eneo hilo majira ya mchana
mwenyekiti huyo alirudi tena ikulu na kufanya mawasiliano na wenzake
waliokuwa kwenye orodha ya kuonana na rais Kikwete na kufanikiwa kuonana
naye.
via>>ITV
No comments:
Post a Comment