Kila mmoja atakubaliana na mimi kwamba mahusiano baina ya wapendanao kwa
kawaida yanakusudia kuwa ya upendo, maelewano, kuaminiana na urafiki wa
hali ya juu ingawa hali halisi siyo hiyo katika uhusiano wa wengi.
Wengi wetu wameumizwa kwa mapenzi. Inawezekana mara moja au nyingi na
hasa kutokana na tatizo la uaminifu katika mahusiano yao.
Zifuatazo nia alama zitakazokusaidia kuwa macho mara utakapoona mazingira ya kufanana nazo yanatokea katika uhusiano wenu.
1.Kuongezeka ghafla kwa hali ya kujipenda.
Yawezekana mpenzi wako alikuwa amezoea kuvaa kawaida, hapa simaanishi
kutopendeza na wewe ulikuwa umemzoea katika halifulani ya mavazi au
mitindo mara ghafla anabadilika na kuwa mtanashati zaidi ana badilisha
mavazi, anapenda mavazi ya garama, labda alikuwa hatumii manukato lakini
gafla anaanza kupenda manukato, anajijali zaidi ya kawaida yake kiasi
ambacho hukumzoea. Katika hali hii jaribu kuwa macho zaidi kufahamu nini
kilicho sababisha mabadiliko hayo..
2.Kuanza kuchelewa kutoka kazini mara kwa mara.
Sio kwamba kila mtu anapochelewa kutoka kazini basi anakuwa sio
mwaminifu, lakini zaidi ya asilimia 75 (kutoka kwenye tafiti) ya ambao
wamekuwa na mahusiano nje wamekuwa wakitoa visingizio vinavyohusiana na
kazi, vikao, mikutano na safari za kikazi, yamkini wewe ni shahidi wa
hili.
3.Anapenda kutembea na mipira ya kinga mara kwa mara (kondomu)
Inashangaza mara nyingine kusikia mpenzi mmoja ana tabia ya kubeba
kondomu kwenye pochi yake au mfukoni kwa kisingizio kuwa anajali cha
kushangaza zaidi unakuta yuko katika mahusiano na mkewe au mumewe.
4.Mazingira tatanishi ya simu:
Gafla simu zinaanza kumiminika mpaka mida ya usiku. Yamkini pia alikuwa
yuko huru hata simu yake inapolia waweza ichukua na kumpatia lakini
gafla anakuwa na hofu kubwa na kuificha simu yake, nimeongea na wengine
ambao wanakwenda na simu hadi bafuni isije ikasikika.
Wengine wanaondoa milio katika simu zao wakati haikuwa kawaida yao, kuwe
siri (password) ngumu hadi mwenyewe anashindwa kuikumbuka, wako ambao
simu zao zikipigwa hawawezi kupokea na kuongea kwa uhuru kama kawaida,
ataondoka na kujitenga pembeni akijifanya anaongea kiuaminifu kabisa.
5.Harufu ambazo hujazizoea:
Kwa kuwa wapendanao huwa wamezoeana, maranyingi hata aina ya manukato
mmoja anayotumia yanakuwa yanajulikana kwa mwenzake, Sasa hembu fikiri
unamkuta mpenzi wako ametokea na ana harufu ya tofauti kabisa na
uliyoizoea, umeisikia harufu hiyo akiwa amerudi toka kazini wakati
asubuhi alipoondoka alikuwa na harufu ile uliyoizoea.
6.Tabia za kuanza kukufuatiliasana au hata kukuganda:
Wapop wanaotawapeleka wapenzi wao kila wanakotaka, nakutoruhusu
mazingira ya wapenzi hawa wakike kuwa huru kufanya mambo yao wenyewe,
wengine waliitafsiri hali hii kama penzi kubwa lakini baada ya muda
unagundua kuwa ile ilikuwa ni ujanja wa kuficha uhalisi wake na kuzuia
mazingira kwa mpenzi wake kugundua au kupewa taarifa ya tabia zake.
7.Mabadiliko katika tendo la ndoa:
Jambo hili linaweza kujidhihirisha katika picha mbili tofauti. Kwa
kawaida wapenzi huwa na mazoea fulani katika tendo la ndoa, kwa muda
waliokaa pamoja kila mmoja humfahamu mwenzake kwa kiasi fulani.
Inawezekana likawa jambo la kushangaza pale ambapo gafla unamuona mpenzi
wako anapoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa, au hata mnapokuwa katika
tendo hilo humuoni akifurahia bali anakuwa kama anayelazimishwa au
kutohamasishwa na chochote.
8.Marafiki wa mpenzi wako kukukwepa:
Inabidi ujiulize sana pale inapotokea gafla wale marafiki wa mpenzi wako
uliowazoea, uliokuwa unawapigia simu wakati wowote leo wana kukwepa na
hata simu hawapokei na mara nyingine wakipokea hawakupi taarifa
yakueleweka au wanakudanganya. Hii yote inawezekana wanamlinda
rafikiyao, au wanakosa cha kujibu maana wanajua uhalisia wa
kinachoendelea.
9.Kuzungumza sentensi za kutatanisha:
Unaweza kukuta katika mapenzi yenu mpenzi wako anaanza kuwa na sentensi
ngumu na zisizo kuwa na msingi kwa mfano anasema “kwa jinsi hii sidhani
kama tutafika” “mi siamini kama mapenzi yanadumu” “yani ndio maana watu
wanashindwa kukaa na mpenzi mmoja” na maranyingine anaweza kukuuliza
baadhi ya maswali moja kwa moja ili kukuona utajibuje. Sentensi hizi
zina chanzo moyoni, kuwa macho.
10.Kuzidi kwa tabia za kutoonekana au kuponyoka:
Gafla sikuhizi haagi anakwenda wapi, ukiuliza inawezakuwa vita. Anakuwa
na vijisafari vingi na vijisababu visivyoisha vya kumuwezesha kuponyoka.
11.Tabia za kuficha fedha:
Hii utaiona ghafla mpenzi wakeo anaanza kuwa na siri kuhusu fedha zake
au matumizi yake, na wala hapendi kuulizwa ulizwa kuhusu suala hilo.
Tabia hii ikidhihirika katika mapenzi yenu usichelewe kuchunguza maana
kwa kukaa kimya unaweza kujikuta umechelea mwana na maji ya moto.
No comments:
Post a Comment