KIMENUKA! Beautiful
Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito shemeji wa
Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana kwa kitendo
cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini Afrika Kusini
‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko linakupa
mchapo kamili.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema na staa wa Bongo Fleva, Omari Nyembo
‘Ommy Dimpoz’ walikwenda Sauz kurekodi video ya wimbo wa msanii huyo
ambao jina lake bado halijafahamika mara moja ndipo baadae picha ya
Ivan, Wema na King Lawrence ilipovuja na kuzua gumzo.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa Sauz, baada ya Wema na Ommy kutua
nchini humo na ‘project’ hiyo ya video, King Lawrance alidaiwa kuandaa
mpango kabambe wa kuhakikisha kwa namna yoyote wanaonana na Wema kisha
kupiga naye picha ambayo akiivujisha mtandaoni kila mtu ataamini
wamefanya malipizi kwa zilipendwa wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye
amemnyakua Zari, mke wa Ivan.
Wema Sepetu (kulia) akiwa na mume wa Zari, Ivan Semwanga (wa pili kushoto), King Lawrance akiwa amemkalia mpenzi wake.
“Ilikuwa ni mpango wa malipizi, King na Ivan walikuwa wanaumia moyoni
kumuona Diamond anatoka na Zari wakati wao wana fedha kuliko Diamond
hivyo waliposikia mtoto wa kike (Wema) yupo Sauz wakasema watadili naye
hadi kieleweke, iwe ni kwa kufanikisha zoezi la kutoka naye kimapenzi au
hata kupiga picha ambazo zikisambaa mitandaoni, watu watajua kwamba
wamefanya malipizi,” kilisema chanzo chetu.
KING AFANIKIWA KUIVUJISHA
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kufanya project, Ommy na
Wema usiku walikwenda katika moja ya klabu kula bata ndipo King na Ivan
walipozama na kufanikiwa kupata picha na Wema wakiwa katika kochi moja
kisha akaitupia katika mtandao wa Istagram.
Wema
aliwachukulia kama washkaji, hakujua jamaa walikuwa na lao kichwani,
walipofanikiwa kupata picha tu, wakaitupia mtandaoni fasta na kufanya
Wema atukanwe na watu,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ACHARUKA
Baada
ya picha za Wema na Ivan kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya
kijamii, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambapo
alimcharukia King kwa matusi mazito ambayo kimaadili hayandikiki
gazetini hata mtandaoni.
“Yule ni...(tusi) ameniboa kweli...(tusi) unajua vitu vingine vya
kipuuzi kabisa, wanatafuta kiki zisizokuwa za msingi wa...(tusi)”
alisema Wema.Wema alisisitiza kuwa hataki kumzungumzia sana King kwani
anaamini akifanya hivyo atamuongezea umaarufu ambao amekuwa akiutafuta
muda mrefu.
King Lawrence amekuwa akimtusi Diamond mara kwa mara kwenye mitandao ya
kijamii huku akionesha jeuri ya fedha kwa kile kinachoonekana kuumia
kwake roho kwa kijana wa Tandale kumchukua shemeji yake Zari, aliyezaa
na Ivan watoto watatu.
No comments:
Post a Comment