17 February 2015
Robo Fainali FA ni Arsenal na Man.United
Hatimaye timu nane zitakazocheza robo fainali za Kombe la FA huko England zimejulikana baada ya kukamilika kwa michezo ya kufuzu kucheza hatua hiyo.
Mabingwa watetezi wa kombe la FA, Arsenal itapambana na Manchester United katika hatua hiyo ya nane bora. Arsenal watasafiri kwenda Old Trafford kuikabili Manachester United katika mchezo wa robo fainali zitakazochezwa tarehe 7 au 8 ya mwezi Machi.
Manchester United ilijihakikishia nafasi hiyo ya hatua ya nane bora baada ya kuishindilia Preston North End mabao 3-1.
Wachezaji wa Manchester United
Mpambano kati ya Arsenal na Manchester United unatajwa kuwa mkali katika hiyo.
Liverpool itakuwa mwenyeji wa Blackburn, Bradford City itapambana na Reading wakati wapinzani wa jadi kutoka West Midlands Aston Villa na West Brom zitamenyana katika uwanja wa Villa Park.
Hatua ya robo fainali kwa timu ya Liverpool itampa matumaini nahodha wake Steven Gerrard kucheza fainali katika uwanja wa Wembley ukiwa ni msimu wake wa mwisho kuwa katika kikosi cha Liverpool, japokuwa watatakiwa kuishinda Blackburn ambao tayari waliwatoa nje ya kinyang'anyiro cha kombe la FA Swansea na Stoke timu za ligi kuu ya England msimu huu.
Steven Gerrard nahodha wa timu ya Liverpool
Timu kutoka daraja la kwanza Bradford imetinga robo fainali za Kombe la FA ikiwa ni mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mwaka 1976, na itakuwa inajiamini kusonga mbele zaidi baada ya kuzichapa timu za ligi kuu za Chelsea na Sunderland katika hatua zilizopita.
Ratiba ya michezo ya robo fainali za kombe la FA inaonyesha kuwa:
Aston Villa watapambana na West Brom, Bradford City na Reading, Liverpool watakuwa kibaruani na Blackburn, huku Manchester United wakipimana ubavu na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Arsenal. Michezo hiyo itachezwa katika siku za mwisho wa juma tarehe 7 na 8
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment