Chazo hicho ambacho kipo ndani ya kampuni hiyo kilisema kuwa pesa hizo zilitolewa na mfanyabiashara maarufu ambaye aliombwa kutoa msaada katika kufanikisha filamu hiyo ambayo ilikuwa iwashirikishe wasanii kutoka Nigeria lakini imeshindikana kutokana na mgogoro wa kiuongozi uliopo kati ya wakurugenzi hao wawili.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa mtu wa kwanza amabaye anaonekana sio muaminifu katika pesa hizo ni Ray kwani mara baada ya mfanyabiashara huyo kukubalia pesa hizo alikuwa akienda kufuatilia msaada kinyemela akiwa na Chuchu huku Johari akibaki ofisini.
Aliendelea kusema kuwa Ray alikuwa akitumia mwanya wa kuwa na mahusiano na Chuchu kwa hiyo hata walipokuwa wakitoka ofisini Johari alikuwa akijua kuwa ni mtoko wa kimapenzi ya kawaida lakini kumbe wao walikuwa wanakwenda kwa mdhamini kuchota pesa za filamu hiyo.
“Baada ya Johari kugundua kuwa kuna mchezo unaochezeka nyuma ya pazia ndipoalipoamua kwenda moja kwa moja kwa mfanya biashara huyo kwasababu yeye ndiye aliekuwa connection ya mchongo huo”.
Gazeti la hilo liliwasiliana na Johari kwa njia ya simu kuhusiana na jambo hilo lakina mara baada ya kupokea simu alisema kuwa yupo kikaoni atafutwe badae.
Kwasasa nipo kwenye kikao siwezi kuzungumzia swa hilo nitafute badae” alisema Johari na kukata simu.Licha ya kutafutwa badae simu yake haikuwa hewani mpaka gazeti hilo linakwenda mitamboni. Ray hakupatikana kabisa kwenye simu.
No comments:
Post a Comment