Miongoni mwa stori zilizochukua headline mitandaoni hata kwenye magazeti
ni kuhusu picha ya hitmaker wa ‘Ndangushima’ Ommy Dimpoz akiwa na ex wa
Diamond Platnumz ,Wema Sepetu kitandani wamelala pamoja na picha
zingine zilizozua mjadala mkubwa.
Ommy Dimpoz amefanya mahojiano na mtangazaji wa Radio Clouds FM kwenye
kipindi cha Amplify ambapo mahojiano yake na mtangazaji huyo 'Millard
Ayo' yalikuwa kama ifuatavyo.
"Ni picha tu mimi naona kama ni picha zingine tu za kawaida, sasa
nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana stori kwasababu
mimi naona sio mara yangu kwanza kupiga picha na Wema hata uki google
utaona tunapicha nyingi sana kwa hiyo sijaelewa kwanini zimeleta stori
May be nafikikiri zilizotengeneza stori zaidi ni hizi ambazo
zinaonesha tuko chumbani kwasababu mimi nilikuwa nimelala kiukweli na
tulikuwa tunakaa kwenye apartment moja nilikua nimeshtukia picha zipo
kwenye mitandao unajua unavyokaa kwenye apartment kwasababu tulienda
kwenye matembezi binafsi na washikaji wengine tulikua wengi wengi kidogo
tulienda South Africa unajua mnavyokaa kama familia kunakuwa na mambo
ya utani utani nimeshtukia tu picha zimeenea kwahiyo hata watu
wakiniuliza ninawambia wamuuliza aliyepiga picha hizo," Alisema Dimpoz.
Millardayo ; “…Wengi wanafahamu kuwa wewe ni mshikaji wa
Diamond Platnumz imekuaje sasa hivi kuonekana kwenye picha na Ex wa
Diamond Platnumz,Wema Sepetu…?”
Ommy Dimpoz ; “…Sidhani kama kuna tatizo kwasababu hawa wote
ni watu wangu nimefahamia nao siku nyingi nimekuwa nao karibu katika
kipindi tofauti kabla hawajakuwa kwenye uhusiano mimi tayari ni watu
wangu sidhani mimi nianze kuelezea sijui ooh nilikuwa labda na Wema
sehemu, Wema ni mshikaji wangu tangia siku nyingi kwa hiyo hata kama
alikuwa katika uhusiano na Diamond yakatokea mahusiano yao pengine
hayapo sasa hivi hayawezi kunifanya mimi kuharibu ushikaji wangu
kwasababu hivyo ni vitu vyao personal…"Alisema.
No comments:
Post a Comment