20 February 2015

Mkurugenzi wa Clouds FM, Joseph Kusaga akanusha redio yake kutumiwa na CCM





- Adai wafanyakazi wake wachache kuwa CCM haimaanishi ni msimamo wa Redio nzima
- Akanusha tetesi za redio yake kununuliwa na Rostam Aziz

 Akijibu swali la Gerald Hando kuhusu na clouds kuhusishwa na CCM amesema Clouds haina chama. Katika mwaka huu wa uchaguzi amesema kila chama kitapewa haki sawa kwenye media yake.

Pia Kusaga alisema media yake imekuwa ikisemwa vibaya hasa na mtandao huu wa JF kuwa clouds ni CCM na amekanusha Na kuita kuwa hizo ni propaganda za wapinzani wake wa media.


Clouds fm wamekana kuwa shutuma zinazotolewa kwenye social media hasa jamiiforums kwamba wao CCM sio za kweli.

Akihojiwa CEO wa clouds katika kipindi power breakfast, amesema wao kama radio hawana chama kwa sababu hata sheria TCRA haziruhusu.

Pia kwenye uchaguzi wa mwaka huu wagombea wote watapewa nafasi sawa.

Ameendelea kusema kuwa wafanyakazi wachache kuwa CCM haimaanishi clouds yote ni CCM.

Pia clouds imekanusha habari zilizozagaa kuwa radio imenunuliwa na Rostam Aziz, ameongeza kuwa hizo ni propaganda za kuichafua radio hiyo.

Amesema kama wakiuza radio watatangaza kwasababu radio ni yao,na hawamuogopi mtu.

Wakati wanamuhoji nimesikia wanamuita Joh (labda ndiye Joseph Kusaga) sina uhakika na majina mengine,wanomfahamu watatujuza.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname