Wakati
akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini
China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’
amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake,
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’, Vanessa Mdee,
Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.
Jack
aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka
2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni
alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani
vya mastaa hao.
MIMBA YA AUNT
Moja kati
ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni
mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza shoo wa
Diamond, Moze Iyobo.
Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani mapenzi hayachagui hasa kama ana furaha.
“Nimeshtushwa
na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na Iyobo…acha apumzike
mapenzi hayachagui as long as ndiyo furaha yake, that’s okey,” aliandika
Jack.
DIAMOND, ZARI
Mbali na
mimba hiyo ya Aunt inayoelekea kuzaa matunda muda si mrefu, modo huyo
alionesha kushtushwa na penzi la staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz
na Zari akishangaa ilikuwaje hadi jamaa huyo akaachana na Wema Sepetu
kisha kutua kwa mrembo huyo mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini na
Uganda.
“Heh! Kwani Diamond aliachana na Wema tena?” Alihoji Jack na kuongeza:
“Sasa
Zari si anakaa South Africa ‘Sauzi’? Wanaonana vipi na Platnumz? Mh!
Wala hawatadumu maana mapenzi ya mbalimbali. Labda kama Nasibu (Diamond
Platnumz) atahamia South.
KAJALA Vs WEMA
Pia video
queen huyo wa Ngoma za Nataka Kulewa (ya Diamond), She Got A Gwan (ya
Marehemu Ngwea) na Kamugisha (ya Linex) aliulizia lile bifu zito la Wema
na Kajala Masanja kama lilikwisha kwani mastaa wa Bongo Movies
walishazoeleka kugombana na kupatana.
Bifu hilo
ni lile la Wema kumtuhumu Kajala kumchukulia bwana’ke (CK) huku
akisahahu kwamba alimlipia Sh. Milioni 13 ili asiende jela miaka mitano
baada ya kukutwa na hatia ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.“Ya Kay (Kajala) na Wema naona
mwishowe watarudisha urafiki tu. Ya Bongo Movies nimeshayazoea huwa wako
hivyo kila muda, kawaida yao.”
JUX, VANESSA
Jack
alipofika kwenye ishu ya kusalitiwa na staa wa Bongo Fleva, Jux akidaiwa
kuwa kwenye malovee na sexy lady wa muziki wa Kizazi Kipya, Vanessa
‘Vee Money’, aliandika ishu hiyo kwa hisia zaidi huku akijilaumu
mwenyewe kwa kosa alilofanya.
“Ya Jux
na Vanessa nimeamua tu kuyaacha coz nipo jela siwezi kumzuia kufanya
lolote then ni makosa yangu yaliyofanya hayo yote kutokea.“Sijui hata
kama itakuja kutokea tena kuwa wote tena mimi na yeye, that chapter
closed already, nahesabia muda mfupi tu now nitatoka lakini sina
chochote cha kufanya nionane naye,” alimalizia kuandika Jack.
Jack
Patrick alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana lakini taarifa zilieleza
kuwa endapo ataonesha nidhamu gerezani ataachiwa mapenzi hivyo hatakaa
jela miaka yote sita.
CHANZO: IJUMAA GAZETI)
No comments:
Post a Comment