Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Master J amekuwa mstari wa mbele
kupaza sauti kuhusiana na kutokuwepo kwa usawa kati ya watayarishaji wa
muziki na wasanii nchini.
Master J ameiambia Bongo5 kuwa kuna watayarishaji ameshaona wanakosa moyo wa kufanya kazi kutokana hali hiyo.
“Tanzania maprodyuza ni maskini, eti wasanii wana hela kuliko
producers hii ni industry gani,” amehoji Master J. “Kwa sababu hapa hizi
sheria zilizopo hazimlindi producer ndo maana anadharaulika. Huyo huyo
msanii yupo tayari akulipe laki mbili umtengenezee wimbo halafu
anauchukua huo wimbo kwenda kutengeneza video kwa milioni 25 yaani wewe
acha tu, hiyo ni dharau kubwa sana,” ameongeza.
“Yaani mimi nikiangalia industry nacheka tu, ni matusi. Huyo huyo
producer unaweza ukamlipa milioni ukishamlipa milioni asikusumbue tena
kwenye revenue share. Yaani unashindwa kumthamini producer hata umlipe
milioni kwa sababu ile laki mbili unayolipia ni studio time lakini
haujanunua haki yangu. Mimi naona pale wewe sasa hivi huangalii hata
Marco ameacha kufanya kazi unafikiria kwanini?"
“Amevunjika moyo yaAni moyo wake umevunjika kabisa kwa sababu
anaonyeshwa laki mbili halafu huyo huyo anayeonyesha lakini mbili
anaenda South Afrika anashoot video ya dola elfu kumi na tano, bila beat
huo wimbo wake utaenda wapi? Bila beat wimbo wako utapigwa r
redioni? Unajua maproducer itafika sehemu watachoka kwa sababu sasa
hivi wengi wameshaanza kuona dharau, kishingo upande wanalalamika.”
No comments:
Post a Comment