STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘AY’ amefunguka kuwa
maprodyuza wengi waliopo Afrika Kusini ‘Sauz’ wanapata faida kubwa sana
kutoka nchi za Afrika hasa Tanzania kupitia muziki.
Akichonga na Over The Weekend, AY alisema wasanii walio wengi kutoka
Bongo wamekubaliana na gharama zao ndiyo maana wanakwenda kurekodi huko
kuanzia ‘audio’ mpaka video.
“Sauz sasa hivi imekuwa kama moyo wa muziki kwa Wabongo kutokana na kila
mmoja kukimbilia huko kwa sababu tu kuna waandaaji wengi wa muziki.
Wanawanufaisha sana, natamani na sisi siku moja Wasauz wakimbilie Bongo
kurekodi,” alisema AY.
No comments:
Post a Comment