Jack.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kilikwenda kumtembelea Jack akiwa
nyuma ya nondo baada ya kuruhusiwa kumuona tangu Machi mosi, mwaka huu,
mwanamitindo huyo amekata tamaa na hana matumaini ya kutoka jela hivi
karibuni.“Aisee Jack Cliff anatia huruma sana, hana matumaini ya kutoka hivi karibuni na ana maumivu ya kupitiliza,” kilisema chanzo hicho.
Jack Patrick akiwa akiwa mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi za heroin tumboni.
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Jack anasema kuwa kesi yake ni
ngumu na endapo atapatikana na hatia, basi atakumbana na kifungo, si
chini ya miaka kumi, jambo ambalo limemfanya kudondosha machozi kila
kukicha huku akituma salamu nyumbani kwao Bongo.
Jack
alikamatwa na unga kilo 1.1 huko Macau, Hong Kong mwezi Desemba, mwaka
jana ambapo sasa kesi yake itaanza kuunguruma Septemba, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment