03 February 2015

Kiwango anacholipwa Lulu kwa kuigiza katika filamu moja, kamshinda hata Ommy Dimpoz anavyolipwa kwa show. Soma hapa


Msanii wa filamu Tanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu katika utafiti uliofanyika tangu mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu,imegundulika kwamba Lulu ndie mwigizaji pekee wa kike anaelipwa hela nyingi kuliko waigizaji wa kike wengine hapa bongo.

Jana tarehe 27/01/2015 katika interview aliyofanya Clouds Tv katika kipindi cha Take One kinachoendeshwa na Zamaradi,Lulu aliweza kutaja dau lake endapo mtu atataka kufanya nae kazi.
Kwa kawaida wasanii wengine wa kike katika filamu wakitakiwa kucheza kama main characters kiwango chao cha kulipwa ni kuanzia laki nane mpaka millioni tano ambapo pia inategemea na makubaliano na producer.
Lakini kwa Lulu ukihitaji kufanya nae kazi aigize kama main character au muhusika mkuu ni anaanzia millioni kumi na tano "15" hiki ni kiwango cha chini ambacho ukihitaji kumchezesha nje na kampuni yake ya Proin Promotions.
Lulu anamiliki kampuni yake mwenyewe inayohusika na utengenezwaji wa filamu zake mwenyewe.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname