Na Musa Mateja/Ijumaa Wikienda
WAKATI mama
mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura
Kasim ‘Sandra’ akiwa nchini India kwa matibabu ya tatizo la kiafya
linalodaiwa kuwa ni kupooza, hapa Bongo dalili za Diamond na mpenzi wake
wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au The Boss Lady kufunga ndoa zinanukia.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari’ au The Boss Lady.
Chanzo
makini kimeliambia Ijumaa Wikienda kwamba, licha ya mama Diamond
kupelekwa India Januari 27, mwaka huu na msafara wa watu wawili, nyuma,
Zari alitua Bongo tangu Januari 30, mwaka huu lengo kubwa likiwa
kumuuguza mama mkwe wake huyo.
ATUA DAR, AENDA SINZA-MORI
Chanzo
kikazidi kuweka wazi kuwa mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Diamond alimpokea na kwenda naye
nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar bila kumwambia kama mama yake
amepelekwa India kwa matibabu.
“Diamond
alikwenda kumpokea Zari lakini hakumwambia kama mama yake amekimbizwa
India kwa matibabu na yeye (Zari) alikuja kwa lengo la kumuuguza mama
mkwe wake,” kilisema chanzo.
BAADA YA KUMKOSA MAMA MKWE
Habari
zaidi zilisema kuwa, walipofika nyumbani na Zari kuambiwa mama Diamond
amepelekwa India, aliumia sana na kumlaumu mpenzi wake huyo kwa nini
hakumwambia kuhusu safari ya mama tangu walipokutana uwanja wa ndege.
‘Zari' akipozi mbele ya magari ya kifahari.
YAISHA, DIAMOND AMPELEKA ZARI KWENYE UJENZI
Baada
ya kuwekana sawa kuhusu usiri wa safari ya mama’ke, Diamond alimchukua
Zari na kumpeleka kwenye nyumba yake anayoijenga Mbezi-Beach, Dar kwa
lengo la kumuonesha sehemu ya mali zake ambapo ilisemekana nyota huyo wa
Uganda aliipenda ramani ya nyumba hiyo.
ZARI AGOMA TENA KULALA HOTELINI
Katika
siku za hivi karibuni, tuliwahi kuandika kuwa Zari alilala kwa mama
Diamond, akapika na kupakua ambapo mawifi zake walimsifia.
Hata
katika ujio wake wa Juni 30, mwaka huu, mrembo huyo mwenye utajiri
mkubwa aligoma kwenda kulala hotelini na kumwambia Diamond atalala naye
nyumbani kwao, Sinza-Mori.
‘Zari' katika pozi jingine.
ZARI AANZA KUBADILI DINI?
Zari
ni Mkristo wa Kanisa la Born Again ambalo ni la kiroho nchini Uganda.
Aliingia kwenye imani hiyo baada kuokoka na kubatizwa kwa maji mengi
kama Biblia inavyotaka lakini kwa kuwa na Diamond kuna dalili za kuanza
kubadili imani ili kutimiza mipango ya ndoa.
“Ukiachia
kwenda kwenye nyumba hiyo ya Mbezi pia Diamond ameshaanza kumfundisha
Zari baadhi ya mambo ya kidini,” kilisema chanzo.
IJUMAA ATINGA BAIBUI
Ijumaa
iliyopita ambayo kiimani, Diamond hupenda kuvaa mavazi ya Kiarabu
ambayo hutafsirika ni ya Kiislam, Zari naye alitupia vazi la baibui ili
kwenda sawasawa na mwandani wake huyo.
Mama yake ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’akiwa katika hali ya ugonjwa.
WAENDA SONGEA WOTE
Wakati
Ijumaa Wikienda likijiandaa kwenda mitamboni, habari za moto ni safari
ya Diamond kwenda mjini Songea ambapo ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma.
Diamond
alikwenda kwa ajili ya shoo ya sherehe za Chama cha Mapinduzi (CCM)
kutimiza miaka 38 tangu kuasisiwa kwake. Sherehe hizo zilifanyika kwenye
Uwanja wa Majimaji jana.
ZARI KWAPANI
Habari za uhakika ni kwamba, katika safari hiyo, Diamond alimuweka Zari kwapani na kwenda naye kwa lengo la kumpa kampani.
DIAMOND: KILA KITU KINA WAKATI WAKE
Ijumaa
Wikienda lilimtafuta Diamond kwa njia ya simu ambapo awali alikiri mama
yake kupelekwa India kwa matibabu. Kuhusu Zari kubadili dini, kuvaa
hijabu na kufunga ndoa, alisema: “Mbona mna maswali sana jamani, kila
kitu kina wakati wake.”
Credit: Gpl
No comments:
Post a Comment