Hii ni mpya kutoka nchini Ghana, zikiwa zimepita siku chache toka timu
ya mpira wa miguu ya Ghana kushika nafasi ya pili katika mashindano ya
AFCON 2015 Rais wao amewakabidhi zawadi alizowaahidi wachezaji wa timu
hiyo.
Rais huyo aliwaahidi gari mpya aina ya Jeep Cherokee ambayo inauzwa
$76,000 za kimarekani ambazo kwa pesa za kibongo ni kama milioni 139
huku pia akiwazawadia kiasi cha fedha $25,000 sana na milioni 45892500
za kibongo.
Raisi wa nchi hiyo amewaomba wawakilishi wa baadhi ya wachezaji wa timu
hiyo ambao wanachezea timu za ulaya wakachukue magari hayo kwa niaba ya
wachezaji hao.
No comments:
Post a Comment