Kama ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye mvuto, wapo pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii ikihitajika Top 10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa umefanya kazi ya kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama ifuatavyo;
10. Elizabeth Michael ‘Lulu’
Binti huyu ana umri wa miaka 21 lakini ni mrembo na anayejiamini. Ni binti kutoka Tanzania mwenye kipaji cha kuigiza kiasi cha kuwa tishio kwa wakongwe. Ni kweli huwa anatumia ‘make up’ lakini hata akiwa hajatumia wala kuvaa ‘mawig’, bado anaonekana ni mwenye kuvutia.9. Omotola Jalade Ekeinde.
Ni mmoja wa mastaa wa kike nchini Nigeria mwenye mvuto wa aina yake. Kwa sasa ana umri wa miaka 37 na watoto wanne lakini bado anaonekana mrembo kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumuita Omosexy.Kutokana na kipaji alicho nacho, amejikuta akiwa na mashabiki wengi katika Bara la Africa na kwingineko duniani. Mbali na uigizaji pia ni mwanamitindo na mwananamuziki.8. Chinyere Yvone Okoro
Huyu ni muigizaji anayetokea nchini Ghana. Katika orodha ya waigizaji wa kike waliomo nchini humo, mrembo huyu amebaki kuwa tishio na imemfanya kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.7. Jackline Wolper.
Huyu ni muigizaji kutoka Tanzania mwenye mvuto wa aina yake. Kwa mujibu wa maelezo yake, uzuri alionao unatokana na mfumo mzuri wa kula aliojiwekea. Anakula sana mbogamboga, matunda na maji mengi, hali inayomfanya autunze urembo alionao.6. Genevieve Nnaji.
Ana umri wa miaka 36, anatokea Nigeria. Mwanadada huyu anatajwa kuwa na mvuto wa aina yake kiasi cha kupata usumbufu kutoka kwa wanaume kibao.Ameigiza filamu nyingi na zote amezitendea haki kutokana na namna anavyouvaa uhusika.5. Jackie Appiah Agyemang.
Amezaliwa miaka 32 nchini Canada lakini amekulia nchini Ghana. Ni binti mrembo na mwenye kipaji ambaye aonekanapo kwenye televisheni, huthibitisha kwamba kuna kitu cha ziada alichojaaliwa na Mungu.4. Nadia Buari.
Huyu ni msanii kutoka Ghana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita. Licha ya umri kusogea, hachuji kwa uzuri. Amecheza filamu nyingi na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kuwa tishio kwenye tasnia ya uigizaji.3. Ini Edo.
Hivi unaanzaanzaje kumuacha mrembo huyu pale unapotaja medemu wakali kwenye tasnia ya filamu Afrika? Naamini huwezi, labda uwe na chuki zako binafsi.Ana umri wa miaka 31 na ana uzuri wa asili unaomfanya atumike kwenye filamu nyingi za Nigeria.2. Stephanie Okereke Linus.
Huyu ni binti kutoka Nigeria ambaye wengi wanamtaja kuwa muigizaji mwenye mvuto kuliko wote Afrika. Ana miaka 33, aliwahi kushiriki mashindano ya urembo nchini Nigeria na kuibuka mshindi. Kuanzia hapo amekuwa gumzo kwa uzuri wake na amekuwa akitumika sana kwenye filamu nyingi.1.Rita Dominic.
Wafuatiliaji wa filamu za Nigeria watakuwa wanamjua vizuri binti huyu. Ana miaka 40 lakini bado anadai. Kila sehemu ya mwili wake ina muonekana wa kiurembo.Angalia midomo yake, angalia macho na ngozi yake. Hakika ni kati ya waigizaji wa kike Afrika wenye mvuto wa aina yake
No comments:
Post a Comment