Staa bei mbaya wa sinema za Kibongo aliyejizatiti katika masomo,
Diana Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi
wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo
Magogoni-Posta jijini Dar.
Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo, mmoja wa wanafunzi wanaosoma na
mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa
akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake
mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.
“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine.
Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.
“Anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa
sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,” alisema mnyetishaji huyo na kusisitiza
kuwa msanii huyo haishi kama supastaa

No comments:
Post a Comment