Mariah Carey na Nick Cannon wanaweza kuwa wanapeana talaka lakini
bado wana jambo la kujibu pamoja kwakuwa wameshtakiwa na yaya wao wa
zamani kwasababu tu alionesha upendo mwingi kwa watoto wao mapacha.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Simonette DaCosta anadai kuwa alikuwa yaya
‘full-time’ wakati watoto hao walipokuwa watoto ambapo aliwalisha,
aliwaogesha na kuwabembeleza lakini hilo halikumpendezesha Mariah.
DaCosta anadai kuwa muimbaji huyo alimkosoa kwa kuwapenda mno wanae hiyo
ikimaanisha kuwa Mariah aliingiwa na wivu sababu watoto wake walimpenda
yaya kuliko yeye.
DaCosta pia anadai kuwa alikuwa akifanya kazi nyingi mno na kudai kuwa alikuwa akitumia saa 100 kwa wiki kufanya kazi.
Anataka alipwe gharama mbalimbali ikiwemo hasara aliyopata.

No comments:
Post a Comment