21 January 2015

Ubaguzi wa rangi, Amber Rose asimulia jinsi familia yake ilivyomtenga kisa Wiz Khalifa ni mtu mweusi

Mrembo Amber Rose ameweka wazi jinsi familia yake ilivyomtenga baada ya kuolewa na Wiz Khalifa.
Rose ameongea kwenye documentary iitwayo Light Girls kuwa baadhi ya ndugu zake hawakuhudhuria harusi yake na Wiz Khalifa kwakuwa aliolewa na mtu mweusi.

Rose mwenye asili ya Creole, Ureno na Italia alieleza kuwa baadhi ya ndugu zake bado wanawatenga watu wenye ngozi nyeusi na wanadhani ngozi yao nyeupe inawafanya kuwa bora zaidi

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname